Taarifa
zinazoihusu Ndege ya shirika la Ndege la Malaysia aina ya Boeing 777
iliyotoweka jana asubuhi bado haijapatikana mpaka sasa ingawa vikosi
mbalimbali vya uokoaji kutoka China vimeelekea huko.Ndege hiyo ambayo inasemekana ilibeba abiria 227 na wafanyakazi 12 kutoka nchi mbalimbali ilipoteza mawasiliano saa moja baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur Malaysia na ilikua ikielekea Beijing China.
Taarifa
zaidi zinadai ndege hiyo ilianguka katika bahari karibu na visiwa vya
Phu Quoc, Vietnam,juhudi za kutafuta ndege hiyo bado zinaendelea katika
visiwa hivyo,baadhi ya ndugu wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo
iliyopotea wameonekana wakilia kwa uchungu mara baada ya kupata taarifa
hizo.
Post a Comment Blogger Facebook