Image copyrightEPAImage captionBrazil imeshindwa kutamba tangu ikose kufana katika Kombe la Dunia mwaka jana
Mataifa mawili yanayojulikana sana kwa kusakata gozi Amerika Kusini yalicharazwa kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia zilizochezwa Alhamisi.
Brazil waliokuwa wakicheza bila nyota wao anayechezea Barcelona Neymar, walilazwa 2-0 ugenini Chile mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia Urusi 2018.
Mambo yalikuwa sawa kwa Argentina waliokubali kichapo cha 2-0 nyumbani kutoka kwa Ecuador, wakicheza bila nyota wao wa Barcelona Lionel Messi.
Chile walishinda kupitia mabao mawili ya kipindi cha pili kutoka kwa Eduardo Vargas na Alexis Sanchez.
Neymar anatumikia marufuku ya mechi mbili za mwisho kati ya nne alizosimamishwa kucheza miezi mitatu iliyopita wakati wa Copa America. Pia atakosa mechi ya wiki ijayo dhidi ya Venezuela.
Mjini Buenos Aires, miamba wa soka Argentina, walikubali kupokea mabao mawili kipindi cha pili kutoka kwa Frickson Erazo na Felipe Caicedo wa Ecuador.
Nyota wao Messi anauguza jeraha la goti na anatarajiwa kurejea uwanjani mwishoni mwa Novemba.
Argentina hata hivyo walikuwa na nyota wengi uwanjani, wakiwemo Angel Di Maria, Sergio Aguero and Javier Macherano.
Kwneye mechi nyingine za kufuzu Alhamisi, Uruguay walilaza Bolivia 2-0 mjini La Paz kupitia Martin Caceres na Diego Godin.
Uruguay walishinda bila Luis Suarez na Edinson Cavani.
Paraguay nao walilaza Venezuela 1-0, bao hilo pekee la mechi hiyo likitoka kwa Derlis Gonzalez dakika ya 84.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova akionyesha silaha kwa waandishi wa habari ...Read more »
H
ere is this year’s edition of the half-yearly round up of our favorite congregational songs. Feel free to add your suggestions in the comments.
...Read more »
Image copyrightReutersImage captionRwanda imo nambari 11 kwenye orodha ya utawala bora ya Mo Ibrahim
Rwanda inaongoza kwa utawala bora katika kanda ya...Read more »
Aliyekua makamu mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, na rais wa CONCACAF ndugu Jack Warner amefungiwa na kamati ya maadili ya sok...Read more »
Kwa mujibu wa madaktari, Messi kukaa nje kwa miezi miwili
Baadhi ya wachezaji wakiwa wamemzunguka Messi kabla ya kupata huduma ya kwanza kwa mad...Read more »
Ratiba ya Ligi Kuu Uingereza wikiendi hii
Ligi Kuu ya Uingereza kutimua vumbi wikiendi hii
Ligi Kuu ya Uingereza inatarajia kutimu tena vumbi ...Read more »
Mayweather akimrushia konde Andre Berto
Floyd Mayweather ameshinda ushindi wa 49 mfululizo kwa alama dhidi ya Andre Berto mjini Las Vegas.
Mpinza...Read more »
Post a Comment Blogger Facebook
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.