0
Paul KagameImage copyrightReuters
Image captionRwanda imo nambari 11 kwenye orodha ya utawala bora ya Mo Ibrahim
Rwanda inaongoza kwa utawala bora katika kanda ya Afrika Mashariki, kwa mujibu wa ripoti mpya kuhusu utawala barani Afrika iliyotolewa na wakfu wa Mo Ibrahim.
Kati ya mataifa 54 barani, Rwanda inashikilia nambari 11 ikiwa na alama 60.7.
Inafuatwa na Kenya iliyo nambari 14 na alama 58.8 kwa mujibu wa ripoti hiyo ya orodha ya Ibrahim Index of African Governance.
Tanzania na Uganda zinafuatana katika nambari 18 na nambari 19 mtawalia. Mataifa hayo mawili hata hivyo yameshuka kwa viwango vya utawala, Tanzania ikishuka alama moja hadi alama 56.7 nayo Uganda alama 1.3.
Rwanda na Kenya zinazoongoza katika kanda hii zimeimarika, Rwanda kwa alama 2.9 nayo Kenya kwa alama 4.3.
Orodha hiyo ilianzishwa mwaka 2007 na wakfu wa Mo Ibrahim kwa lengo la kugeza hatua zinazopigwa na mataifa ya Afrika katika kuimarisha utawala.
Ripoti hiyo iliangazia sana mambo manne: Usalama na Utawala wa Sheria, kushirikishwa kwa wananchi na haki za kibinadamu, fursa ya kuendeleza hali ya kiuchumi na maendeleo ya binadamu.
„Matokeo ya 2015 kwa jumla yanaonyesha ingawa kwa jumla Waafrika wana afya bora na wanaishi katika mataifa yenye demokrasia zaidi kushinda miaka 15 iliyopita, upigaji hatua katika nguzo nyingine za utawala bora barani umekwama,” alisema mwenyekiti wa wakfu huo Bw Mo Ibrahim.
Burundi inashika mkia ikiwa nambari 38 na alama 45.8, ikiwa imepanda kwa alama 1.2.
Taifa linaloongoza barani Afrika ni Mauritius lililo na alama 79.9 na linaloshika mkia ni Somalia na alama 1.2.

Post a Comment Blogger

 
Top