0



Image captionEdward Lowassa alizaliwa August 26 mwaka 1953 kijijini Ngarashi Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.
Edward Ngoyai Lowassa anatoka katika ya jamii ya wafugaji Kaskazini mwa Tanzania.
Alizaliwa August 26 mwaka 1953 kijijini Ngarashi Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.
Kitaaluma Lowasa ni msomi , akiwa na shahada kwanza kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam na shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Bath huko Uingereza (1983-1984).
Uzoefu katika siasa
Edward Lowasa ni mtoto wa tatu wa Mzee Ngoyayi.
Ingawa baba yake alikuwa mfugaji aliwahi pia kufanya kazi kama tarishi katika serikali ya wakoloni.
Image captionLicha ya kuwa mwanachama wa CCM kwa miaka 38, bwana Lowassa aliwashangaza wanachama wa CCM kwa uamuzi wake wa kukihama chama hicho.
Alijiunga na chama cha CCM mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka wa 1977.
Kabla ya kugombea ubunge , aliwahi kutumikia jeshi la Tanzania na hata kupigana katika vita kati ya Tanzania na Uganda vilivyopelekea Idd Amin kuondolewa madarakani.
Baada ya hapo alikuwa mtumishi wa umma kwa miaka kadhaa kabla kuteuliwa kuwa mbunge kuwajilisha vijana na kujiunga rasmi na siasa.
Mwaka wa 1990 alijitosa ulingoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la uchaguzi la Monduli.
Alifanyikiwa kwa miaka yote hii Lowassa ameendelea kulishikilia jimbo hilo la uchaguzi hadi sasa anapolazimika kuliachia ili kuwania Urais.
Hii si mara yake ya kwanza kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kwani mwaka 1995,alikuwa miongoni mwa watangaza nia 15, hata hivyo nafasi ikachukuliwa na Benjamin William Mkapa.
Image captionNi mshika bendera wa UKAWA ambao ni muungano wa vyama vinne vya upinzani
Hata hivyo tofauti na matarajio ya wafuasi wake, Mwaka 2005, Lowassa hakuwania nafasi hiyo, badala yake aliunga mkono rais anayemaliza muda wake Jakaya Kikwete.
Je Lowassa huyu wa sasa amewahi kuwa nani katika nyadhifa alizozipitia kiserikali?
Edward Ngoyayi Lowassa amewahi, kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, Ardhi na Maendeleo ya Makazi pamoja na nafasi nyinginezo.
Lakini pia nafasi za juu alizowahi kuzipata ni pamoja na kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka Febuari 7 mwaka 2008, alipolazimika kujiuzulu baada ya madai ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa ya Kampuni ya Richmond, Madai ambayo bwana Lowassa aliyakanusha hadi sasa.
Katika siasa,Lowassa anafahamika kama mtu wenye misimamo mikali,kwa kile anachokiamini mwenyewe kama siasa zinazo ambatana na maamuzi magumu.
Licha ya kuwa mwanachama wa CCM kwa miaka 38, bwana Lowassa aliwashangaza wanachama wa CCM kwa uamuzi wake wa kukihama chama hicho.
Image captionKufuatia uamuzi wake wa kubadili chama, Edward Lowasa amelazimika pia kubadili msimamo wake wa kisiasa
Hatua iliyochangiwa na yeye kutoridhrishwa na jinsi uteuzi wa wagombea urais wa kilichokuwa chama chake ulivyoendeshwa.
Alijiunga na chama cha kikuu cha upinzani cha CHADEMA.
Hiki ni mojawapo ya vyama vinne vya upinzani vinavyounda umoja uitwao,UKAWA.
Kufuatia uamuzi wake wa kubadili chama, Edward Lowasa amelazimika pia kubadili msimamo wake wa kisiasa na kuwa mpinzani wa chama tawala na sera aliziunga mkono na kuzitumikia awali, jambo ambalo linawatatanisha wakosoaji wake .
Hii ni mara yake ya pili kujaribu kuingia ikulu.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment Blogger

 
Top