Muda mfupi baada ya mchezo wa jana wa ligi kuu ya England kati ya Arsenal na Liverpool ambao uliisha kwa matokeo ya Liverpool kuichapa Arsenal 5-1, kipa wa klabu ya Arsenal Wojciech Szczesny alitumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii kuwaomba msamaha mashabiki wa timu hiyo kwa kipigo hicho.
Aliandika: “Ilikuwa ni aibu kubwa, samahani kwa yoyote aliyekaa dakika zote 90 kuangalia hiyo mechi” 
Post a Comment Blogger Facebook