|
|
|
|
LILE jambazi linaloua watu wasio na hatia Tarime, Mara lipo katika
wakati mgumu kufuatia wananchi wa wilayani humo kumfungia kazi kwa
kumsaka licha ya Jeshi la Polisi Tanzania, Makao Makuu kutuma askari
wake kwa ajili ya kumsaka.
Kwa mujibu wa chanzo chetu Tarime, wananchi wamesema wamechoka kuona mdunguaji huyo anaendelea kutamba kwa kutoa roho za watu kama ninja.
“Wananchi wengi hapa Tarime nao wameanza kuingia mitaani kumsaka. Wamekasirika sana na wanasema wakimkamata wataanza kumkata kiungo kimoja baada ya kingine hadi aache kuhema (afe) ili na yeye aonje tamu ya kuua,” alisema mwananchi mmoja alipozungumza na Ijumaa.
Mwananchi mwingine alisema kuwa, raia wenye silaha zao ndani nao wameamua kuanza kutembea nazo kwa ajili ya kumsaka jambazi huyo ambaye licha ya kuua, hachukui mali zaidi ya chakula.
Mpaka sasa, ‘jitu’ hilo kwa kutumia bunduki aina ya SMG limeshaua na kuacha majeruhi kibao katika vijiji vya Mogabiri na Nkende.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi Tanzania, Paul Chagonja alisema juzi kuwa, muuaji huyo inasadikiwa si mkazi wa eneo hilo.
Alisema sababu ya mtu huyo kufanya mauaji hayo haijulikani kwa vile baada ya mauaji hachukui mali isipokuwa vitu vidogo kama simu za mkononi, mikate, biskuti na soda.

Post a Comment Blogger Facebook