0
Ukitoa sehemu ambazo umekwisha zisikia kuwa zimegundulika nishati ya Gesi unaambiwa Kampuni ya Statoil ya Norway na mshirika wake ExxonMobil wamegundua kiasi kingine kikubwa cha gesi katika Bahari ya Hindi.

Kwa mujibu Statoil wamedai kuwa Kiwango hicho kinakadiriwa kufikia futi za ujazo trilioni mbili mpaka tatu (sawa na lita trilioni 56.6 hadi trilioni 84.9).
Ugunduzi huu unafanya jumla ya ujazo wa gesi iliyogunduliwa na washirika hao kufikia takriban futi za ujazo trilioni 20 (lita trilioni 566.25) kwenye Kitalu Namba 2, ambako washirika hao wanafanya shughuli za utafiti na uchimbaji.
Makamu wa Rais kwa shughuli za utafiti wa Statoil ukanda wa Magharibi ndugu Nick Madem amesema>>’tangu mwaka 2012 tumekuwa tukipata mafanikio ya asilimia 100 nchini Tanzania na eneo hilo limekuwa kitovu cha utafiti ndani ya muda mfupi’
Nick Madem ameongeza kwa kusema>>’Ni kwa haraka tulitoka kwenye kuchimba kisima kimoja hadi kuwa na mkakati wa kuchimba visima vingi’.
Ugunduzi huo mpya katika Kisima Piri-1 umefanyika katika eneo lenye kiwango kidogo cha mawe ya mchanga kama ilivyokuwa wakati ilipogunduliwa gesi katika Kisima cha Zafarani-1 mwaka 2012.
Ugunduzi katika kisima hicho unakuwa wa sita katika Kitalu Namba 2,uchimbaji wa gesi katika kisima hicho ulifanywa na meli ya Discoverer Americas,usawa wa mita 2,360 za kina cha maji. Meli hiyo sasa inachimba kisima kingine cha Binzari katika Kitalu namba 2.
Statoil ambayo imekuwapo Tanzania tangu mwaka 2007 ambao wamkua wakifanya utafiti na kuchimba gesi katika kitalu namba 2 kwa niaba ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ikiwa na hisa ya asilimia 65 katika kitalu hicho wakati ExxonMobil Exploration and Production Tanzania Limited ina asilimia 35.
Source:Mwananchi.

Post a Comment Blogger

 
Top