0
Linex na Zitto

Linex amepewa sapoti kubwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ili aachie audio na video ya wimbo wake unaoitwa Wema kwa Ubaya...>>>

Linex ameeleza kuwa Zitto Kabwe alimpa idea ya kufanya wimbo ambao angeusapoti lakini Linex akagundua kuwa ana wimbo alifanya mwaka jana na una hisia na ujumbe utakaosaidia kuwapa faraja wengi wenye matatizo, alipomfikishia mheshimiwa aliukubali.
Zitto alivutiwa na ujumbe wa wimbo huo unaohusu watu kutolipiza kisasi na kuendelea kumtegemea Mungu katika kila jambo. Baada ya kuguswa alimfuata Adam Juma na kulipia video hata bila kumwambia Linex, baadae akampa taarifa ajiandae kushuti.
“Tunaanza kushuti next week kwa sababu nilikuwa bado niko busy na Kili Tour. Ni wimbo mzuri utakaoigusa sana jamii halafu baadae tukishashuti tutajua mambo mengine.”

Post a Comment Blogger

 
Top