0

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu wameshambulia kituo cha polisi na mahoteli na vijiji mjini Mpeketoni, pwani ya Kenya .
Makabiliano makali yameripotiwa sehemu kubwa ya Jumapili usiku huku wakaazi wakitorokea maeneo ya msitu karibu na kisiwa cha Lamu..
Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa hadi kufikia sasa watu 48 wanahofiwa kuuawa kartika shambulizi hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo vyombo vya habari vinasema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Shambulizi lilifanyika usiku wa kuamkia leo watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao wakiwa wamejihami vikali walivamia vituop vya polisi , hoteli na benki.
Shambulizi hilo linakuja siku kadhaa baada ya serikali ya Uingereza kufunga ofisi zake kwa hofu ya usalama.

Duru za jeshi la Kenya zimearifu kuwa wapiganaji hao hawajajitambulisha ni wa kundi gani.
Baadhi ya walioshuhudia wamearifu BBC kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.
Kenya imekumbwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa kisomali wa Al Shabaab tangu ipeleke wanajeshi wake ndani ya Somalia mwaka wa 2011.
Duru kutoka kisiwa cha Lamu zimearifu kuwa wapiganaji hao walifika katika malori mawili na kurusha kifaa kama bomu ndani ya kituo cha polisi kisha wakavamia na kuiba silaha.
Kituo kimoja cha polisi kilichoshambuliwa na wapiganaji hao
'Washambuliaji ni kina nani ?'
Msemaji wa Jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir ameandika katika mtandao wa Twitter kusema kuwa wapiganaji hao wameshambulia kijiji kimoja na kufyatua risasi kiholela katika kituo kikuu cha biashara.
''Huenda wapiaganji hao wakawa Al shabaab,'' ameongeza Major Chirhir.
Usiku wote ndege za polisi zimepaa eneo la Mpeketoni hadi Lamu kudadisi hali ilivyo huku polisi wakikabiliana vikali ardhini. Kamanda mkuu wa kaunti ya Lamu ameondoka na maafisa zaidi wa polisi kusaidia makabiliano yanayoendelea huko.
Mmoja wa walioshuhudia amesema kuwa mahoteli yameshambuliwa. "baadhi ya mahoteli yamewashwa moto hatujui watu wangapi wamejeruhiwa kufikia sasa. Tumeambiwa wameshatoroka lakini polisi wanawafuata waliko,'' ameongeza.
Lamu , Kenya
'Kivutio cha watalii'
Kisiwa cha Lamu kilichoko karibu sana na eneo hilo ni maarufu sana kwa shughuli za kitalii katika eneo hilo la Afrika, huku likiwa na majengo ya kale zaidi na kihistoria ambayo yameorodheshwa na shirika la Unesco kama turathi ya kimataifa.

Post a Comment Blogger

 
Top