Mfanyakazi wa White House (Ikulu ya Marekani) alikamatwa na kupewa likizo isiyo na malipo baada ya kutuhumiwa kunyakua bunduki ya mpenzi wake na kumfyatulia risasi wakati wa malumbano makali, polisi walisema Jumatatu.
Barvetta Singletory, 37- msaidizi maalumu wa Rais na masuala ya kibunge Ikulu – alikamatwa Ijumaa baada ya tukio hilo.
Aliripotiwa kumshambulia mpenzi wake, afisa wa polisi wa Capitol Hill, ambaye alimuona msichana mwingine kabla ya kukwapua simu zake mbili na bunduki ya 40 caliber, NBC iliripoti.
Post a Comment Blogger Facebook