0

Bale akipiga kichwa kuifungia Wales goli dhidi ya Cyprus kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Ulaya uliochezwa Alhamisi usiku.
Bale akipiga kichwa kuifungia Wales goli dhidi ya Cyprus kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Ulaya uliochezwa Alhamisi usiku.
Gareth Bale amethibitisha kuwa Wales bado inanafasi ya kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Ulaya baada ya kuifungia goli la dakika za lala salama na kuipa ushindi wa goli 1-0 wakati ikicheza na Cyprus jana kwenye mechi ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya Ulaya mwaka 2016.
Kiungo wa Wales David Edwards alifunga goli ambalo lilikataliwa kabla ya Neil Taylor hajapoteza nafasi nzuri kipindi cha kwanza kilichomalizika kwa sare ya bila kufungana.
balaBale alifunga goli hilo kipindi cha pili dakika ya 82 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Jazz Richards na mpira kutinga moja kwa moja kwenye nyavu za juu za Cyprus na kufungulia sherehe kwa mashabiki wa Wales waliosafiri kwenda Cyprus kuishangilia timu yao.
ga1
Wales inaendelea kushikilia rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja kwenye Kundi B ikiwa na uhakika endapo itashinda mchezo wake wa Jumapili dhidi ya Israel itakuwa imefuzu kucheza michuano ya mataifa ya Ulaya ikivunja historia mbovu ya kushindwa kufuzu kwa takribani miaka 57 iliyopita.
Matokeo ya mechi nyingine za kufuzu kucheza michuano ya Ulaya zilizopigwa jana ni kama ifuatavyo;
ga2

Post a Comment Blogger

 
Top