Mara nyingine husemekana kwamba ulaji wa ndizi nyingi kupita kiasi kwa mpigo unaweza kuhatarisha maisha yako.
Imedaiwa zaidi kwamba ulaji wa zaidi ya ndizi sita kwa mpigo unaweza kukuuwa.
Je, hili ni kweli?Ndizi ni mojawapo ya matunda yenye umaarufu mkubwa duniani yenye vitamini na madini.
Kwa upande huo ndizi huonekana kuwa na manufaa makubwa kwa mwili wa binaadamu,kwa hivyo basi kwa nini watu huwa na fikra kwamba matunda hayo yanaweza kuwa hatari na hata kuuwa?
Mmoja ya watu maarufu ambao wamekuwa wakisambaza ujumbe huo ni Karl Pilkinton rafikiye msanii mcheshi Ricky Gervais.
''Awali wakati mulipokuwa mukizungumza kuhusu ndizi ,nilikuwa na hakika kwamba unapokula zaidi ya ndizi sita unaweza kufariki'',alisema katika mazungumzo yake na Gervais na msanii mwenza wa vichekesho Stephen Merchant.Ni Kweli.
Madini ya Potasiam yaliomo katika ndizi ni ya viwango vya juu na ni hatari iwapo tayari umekula ndizi sita.
''Niliona bakuli lililojaa ndizi na lilikuwa na ndizi sita pekee ,unajua kwa nini ni ndizi sita ndani ya bakuli hilo,kwa sababu ndizi saba ni hatari''.
Je, madini ya potosium yana hatari gani? Kwa kweli ni muhimu katika maisha ya mwanadamu na hupatikana katika seli zote za mwili wa mwanadamu kulingana na mtaalamu wa chakula Catherine Collins kutoka hospitali ya St George's mjini London.
''Tunatumia kuzalisha umeme ndani ya mwili wa mwanadamu ambao husaidia seli hizo kufanya kazi vizuri.Inasaidia katika kuweka viwango vya moyo kuwa kati hali nzuri mbali na kusaidia kudhibiti sukari ndani ya damu pamoja na kuhimili presha''.
Na iwapo viwango vya madini hayo viko chini mno ama hata juu zaidi inaweza kuathiri viwango vya moyo,maumivu ya tumbo,kusikia kisunzi na hata kuhara.
Utumiaji wa madini ya potasiam kloraid kwa kupitia kiasi kunaweza kusababisha mshtuko wa moyo.
''Lakini kwa mtu mwenye afya ,sio rahisi kufariki kwa kula ndizi zaidi ya sita'' ,alisema Collins.''Itahitajika kula zaidi ya ndizi 400 kwa siku kwa wewe kuweza kujenga viwango vya madini ya Potasiam ambayo yatasababisha moyo wako kusita kupiga.Ndizi hazina hatari, na kwa kweli ni nzuri sana kwa
Post a Comment Blogger Facebook