0

Nimeshapigwa sana mkwala na jumbe za vitisho,
ila siamini huu msafara ni vibaraka wa Mrisho,
si tulianza sawa vita ya kuitetea Ikulu?
Leo umeisaliti UKAWA kwenye sherehe za uhuru!
Uhuru uko wapi mnasherekea uhuru!?
Uhuru wa kutowafilisi viongozi wakijiuzulu?
Na wanaokufa maskini wanangu wa Burya Nkulu,
Mungu aliwapa madini mnambinafisisha Mkaburu!
Bungeni sioni kinachoendelea,
naona wasomi wakisutana umbea,
wengine walishikwa ugoni picha zilienea,
hamuwaoni jimboni afu bado mnawalea!
Mambo ya…. Spika anabadilisha mada,
akiona chama tawala amezalilishwa kada!
Spika wa Bunge ona analinda watu wa chama chake,
na bunge ni la watu wote siyo chombo cha watu wachache!
Safari ya Rais eti Tume inaundiwa Tume,
wakati Mwananyamala wanatibu Tezi dume!
Kadi ya chama nachana, nanyongea ganja navuta,
nikamateni si mlimshindwa Tibaijuka?
Leta Defender, leta Wajeda, leta Wagambo Roma nimejitoa sadaka.
Na mkitaka kuniua hiki kichwa sifii hapa,
nichinjeni mkanitupe kwenye daraja la Mkapa..
Mother**** Walafi wa madaraka,
hata Nyerere, Gaddafi si walikufa kwa mashaka?!
So hakuna kiongozi msafi, je nani mwenye mamlaka,
anitajie mtoto wa Rais anayesoma shule ya Kata!

VIVA ROMA VIVA X4
Katiba ni sauti ya umma na kuna uhuru wa kuongea.
Na nyie si ndio mmenituma, mpo tayari kunitetea?
Wilaya mnafanya Mkoa ili wapangwe washikaji,
Mkuu wa Wilaya Changudoa hii ni miradi ya upigaji!
Watasafirisha Nyani, sisi tunashangaa Twiga?
Utamfunga nani yeye na Mwanasheria Mkuu ni maswahiba,
na wasanii tuombee Rais ajaye asipende tu vikuu,
wataalikwa wapemba hatutamuona hata Lukuvi!
Unampigiaje Kura Fisi awaongoze Mbuzi,
kwa hongo ndogo ya kipisi unampa Ikulu mlanguzi!
Geita mlinyimwa dhahabu watawalaghai kwa vitenge,
napata kwa gadhabu propaganda za wabunge wasee**** ngerema
Ukistaajabu ya Lema utayaona ya Mrema,
ona pepo la usaliti linaitafuna CHADEMA,
kwetu Rais ni taasisi inayochaguliwa na mfumo,
sisi wawakilishi na kwenye maamuzi hatumo!
Watoto wao wanauza Ngada, Baba Fisadi, Mama anafanya Ukahaba, yupi mwema kiitikadi?
Na vita ya Mahakama ya Kadhi ni uhasama wa wazi,
yaani unaisaka bikra ndani ya wodi ya wazazi?!!
Nipige risasi ya utosi si ndo nidhamu ya utawala,
maana waliomuua Mwangosi waliongezewa mshahara,
Dr. Mvungi Ona dah! Wakamzawadia jeneza,
na hawafungwi! Nipe case nitaimba ndani ya gereza..

(Peperusha Bendera, VIVA ROMA VIVA)

Mbona mama yako anauza gongo, na gongo ndio iliokulea hadi leo umekuwa polisi, na humpeleki Segerea, life is not fair
Polisi mna maisha gani? Mnakufa maskini kwa kuwatetea wanyang’anyi!
(Peperusha Bendera, VIVA ROMA VIVA)
Hakuna mtoto asiye na mzazi yupi wa serikali ya tatu?
Mikataba iweke wazi Demokrasia ni watu,
ona sasa kila msomi anaikimbilia siasa,
nchi itajengwa na nani? Ajira imekuwa serious!
Wanafanya biashara haramu , bado hawalipi kodi, nani atahoji, na hao ndio Wadhamini wa Bodi!?
Jasho analila Mzungu wachimbaji wadogo wa Migodi, au mnataka Ivan aje awe mfuasi wa Panyaroad?!
Pesa sherehe za Muungano amzingatii Itifaki,
wanafunzi mnawachoma jua na shule hawana madawati,
mnalipa mishahara hewa, na hamlipi mafao walimu,
na mlimpiga Warioba alivyowaletea Rasimu!
Nchi inalima, Pamba nyinyi mmeua Viwanda,
tunauzia wawekezaji ona Dola inapanda!
Tunageuka waagizaji kisha wanatuuzia mitumba,
uchumi unayumba leta fujo upigwe kama Lipumba!
Na kutabiri nani afuate? Karibu Tanga kunani …
Round hii kombe linaenda Monduli? (Masai yellow subhai) …
Au Kombe ni la Magufuli? Kama kawa kama dawa, Je, Kombe linabaki UKAWA?!
Mmarekani anataka Wese (we hakuna atakayepona), Na mchina akifuata gesi? Mwambie nangwanda sijaona..
VIVA ROMA VIVA..

Post a Comment Blogger

 
Top