Kundi la watoto wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania ambao mikono na miguu yao ilikatwa na waganga wachawi wamerudi kutoka Marekani wakiwa na viungo bandia.
Watoto watano walisafirishwa hadi Hospitali ya Watoto ya Shriners iliyopo Philadelphia mwezi Juni kwa ajili ya matibabu ya majeraha ya kikatili waliyoyapata na hivyo kuwekewa viungo bandia.
Wa kwanza kati yao ni Kabula Nkarango Masanja, 17, amerudi nchini Tanzani, na kuwaambia madaktari wa Marekani na wafanyakazi jamii wa Tanzania kuwa: “Mungu awe nanyi”.
Walemavu wa ngozi wanafanyiwa ukatili nchini Tanzania na waganga ambao wanaamini viungo vyao vinaleta utajiri na bahati.
Kila mwaka mlemavu wa ngozi hutekwa na kukatwa viungo vyake, nywele zake, meno na hata nyeti zake hukatwa na mapanga ili kutumika kuleta bahati na kuuzwa kwa bei aghali.
Montanti, ambaye anaishi karibu na nyumba ya hisani ya “Dare to Dream”, ametumia miaka mingi kusafirisha watoto waliopoteza viungo kutoka maeneo mengi yenye ukatili huo yakiwemo Bosnia, Haiti, Iraq, Afghanistan, Libya na Syria.
Post a Comment Blogger Facebook