0
Viumbe sawa na binadamu vyapatikana AK

Wanasayansi nchi Afrika kusini wamevumbua masalia mapya yafananayo na binaadamu katika pango fulani nchini humo.

Masalia hayo yenye vipande kumi na vitano ni uvumbuzi mkubwa kuwahi kuonekana kwa masalia barani Afrika.

Masalia hayo baadhi ni ya binaadamu na baadhi ni kama ya sokwe lakini wanasayansi hao wanaamini na kudai kuwa ni kati viumbe hivyo viwili.
Image captionMabaki yaliyopatikana Afrika Kusini

Kupatikana kwa mabaki hiyo ya mifupa ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana barani Afrika.

Watafiti hao wanasema kuwa ufumbuzi huo utabadili mawazo kuhusu binadamu walioishi miaka ya zamani.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Elife, umebainisha kuwa viumbe hivyo vilikuwa na uwezo na tabia ya kutoa tambiko.

Image captionWanasayansi waliofumbua mabaki haya

Viumbe hivyo sasa vimepewa jina la Naledi na vimejumuishwa kwenye kundi moja na binadamu.

Hata hivyo watafiti hao hawajasema na kubainisha ni miaka mingapi viumbe hivyo viliishi, lakini mtaalumu mkuu, Prof. Lee Berger ameiambia BBC kuwa anaamini viumbe hivyo ni miongoni mwa vizazi vya kwanza vya binadam na huenda viliishi barani Afrika takriban miaka milioni tatu iliyopita.

Post a Comment Blogger

 
Top