0
Marufuku ya kuvuta sigara mjini Lagos
Wabunge mjini Lagos, wamepitisha sheria inayoharamisha uvutaji sigara katika maeneo ya umma, ikiwemo mikahawani na katika maeneo ya usafiri wa umma.
Wale watakaopatikana na hatia ya kupuuza onyo hilo, huenda wakatozwa faini ya dola 62 au kufungwa jela miezi mitatu
Mswada huo unaharamisha uvutaji sigara mbele ya watoto na watakaopatikana na hatia watatozwa faini ya dola 94 au kuhukumiwa jela mwezi mmoja.
Mji wa Lagos tayari umewapiga marufuku madereva wa magari ya usafiri wa umma kuvuta sigara wakati wakiendesha magari, ili kuimarisha usalama barabarani.
Lagos ni moja ya miji mikubwa Afrika huku idadi ya watu ikitarajiwa kuongezeka hadi watu milioni 12 ifikapo mwaka 2015 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Lakini maafisa wa mji huo wanasema kuna watu milioni 21 mjini humo.
Mswada wa Marufuku ya uvutaji sigara mjini Lagos, utakuwa sheria pindi utakapotiwa saini na gavana wa jimbo hilo, Babatunde Fashola.
Mwandishi wa BBC mjini Lagos Tomi Oladipo, anasema kuwa tayari uvutaji sigara umeharamishwa na serikali kuu lakini utekelzwaji wa sheria ni dhaifu sana.
Mjini Lagos uvutaji sigara hufanyika sana katika baa, mikahawa na vilabu.

Post a Comment Blogger

 
Top