Russian Socialite ambae ni muhariri wa jarida la Garage magazine,
Dasha Zhukova akiwa pia ni patner wa mmiliki wa club ya Chelsea Roman
Abramovich, ameingia kwenye maporomoko ya matusi na maoni mengine mazito
ya watu mbalimbali mtandaoni baada ya kusambaa kwa picha inayomuonyesha
akiwa amekaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa mfano wa Mwanamke wa
Kiafrika.
Mwanamke huyu ambae anasema ana mapenzi na fashion pamoja na usanii
wa vitu kama hivi amekosolewa na wengi ambapo baadhi ya Wanawake hata
wenye ngozi kama ya Dasha, wamemkosoa huku wengine wakiuliza ‘bado
tunafanya vitu hivi mpaka huu mwaka wa 2014?’Kiti hiki kimedizainiwa na msanii raia wa Norway Bjarne Melgaard ambapo
baada ya kupostiwa kwa picha hii kwenye mitandao akiwa anafanyiwa
interview na tovuti ya Buro 24/7 , muda mfupi baadae waliitoa hii picha
na kuomba radhi kwa kitendo hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment Blogger Facebook