0

Kwa mujibu wa BBC, mnamo mwaka 2012 Nov walitoa makala ya kumuonesha rais Jose Mujica ambaye ni rais wa Uruguay anayesadikikika kuwa ndiye Raisi masikini kuliko maraisi au viongozi wote wenye nyadhifa kubwa duniani.

Jose Mujica, inasemekana ni masikini kutokana na kipato chake ambacho asilimia 90 anatoa msaada na 10% kinamtosheleza kuendesha maisha yake yeye na familia yake.
Gari lake la kutembelea
Raisi huyo ambaye ameonekana akiishi maisha tofauti kabisa na marais wengine wanavyoishi, kwa namna yake anaishi kwenye shamba akiwa na mke wake ambaye ndiyo mmiliki halali wa sehemu wanapoishi baada ya kuwaachia viongozi wengine sehemu alipojengewa na selikari na kwenda kuishe huko kijijini nje kidogo na jiji la Montevideo nchini Uruguay, ana ulinzi wa askari polisi wawili na mbwa wake watatu. Mzee huyo amesema anafurahia sana maisha anayoishi kwakuwa yuko huru zaidi ukiringanisha na maisha ya viongozi wengine

Post a Comment Blogger

 
Top