Aliyekua makamu mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, na rais wa CONCACAF ndugu Jack Warner amefungiwa na kamati ya maadili ya soka ya FIFA kutojihusisha na masuala yote yahusuyo soka katika maisha yake yote.
Hali hiyo imetokana na uchunguzi uliofanywa na tume ya uchunguzi kuhusiana na uhusika wake katika upigaji kura wa nani awe mshindi wa maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2018/2022.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ndiye mrithi wa Warner, Dr. Cornel Borbely alianzisha rasmi uchunguzi huo mwezi Januari mwaka huu.
Jack Warner amekutwa na hatia ya kujihusisha na masuala makubwa ya FIFA na CONCACAF pasipo ueledi huku pia akiwa anahusika na rushwa na utovu wa nidhamu.
Katika nafasi yake, Warner alikua ndiye anayepitisha mikataba, usajili na mambo yote yahusuyo pesa kwa siri. Kamati ya maadili ya soka imejiridhisha kumpa adhabu hiyo iliyoanza rasmi 25 September 2015
Post a Comment Blogger Facebook