SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA KAMANDA MOHAMED MTOI KANYAWANA
Nachukua fursa hii kwa masikitiko makubwa sana kutoa Salamu za Rambirambi kwa Familia na Uongozi wa Juu wa Chadema Makao makuu kwa msiba wa Kamanda mwenzetu, Mpiganaji wa kweli, Kijana mwenzetu Ndugu Mohamed Mtoi Kanyawana aliyefariki kwa ajali ya Gari iliyotokea huko Tanga.
Kwa kweli bado tulikuwa tunamhitaji sana kamanda mwenzetu lakini kifo ni mpango wa Mungu ametangulia mbele sisi tupo nyuma yake. Tunajua mchango wake wa kujenga Chama na tunauthamini sana.
Mohamed Mtoi alikuwa ni tegemeo letu kwenye nafasi ya Ubunge Jimbo la Lushoto pia kama mratibu wa Kanda ya Kaskazini, hivyo tumepata pigo kubwa sana hasa katika kipindi hiki kigumu kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Tulikuwa tunashirikiana sana na Ndugu Mohamed Mtoi kwenye kusambaza Taarifa Mbalimbali za Chama, mchango wake ulikuwa mkubwa sana. Mungu aiweke roho ya Marehemu Mohamed Mtoi Kanyawana mahali Pema Peponi.
Chanzo: Chadema Blog
Post a Comment Blogger Facebook