0
Diwani wa Isakamaliwa, Igunga, Doto Kwilasa, Ofisa Mtendaji wa Kijiji, Erasto Shokoro, wajumbe sita wa serikali ya kijiji na mtu ambaye hajajulikana wamenusurika kuchomwa moto na wananchi.
Wananchi hao waliwafungia ndani ya chumba cha mikutano viongozi hao kwa madai ya kuitisha kikao cha kuwazuia vijana wa Isakamaliwa wasilipize kisasi kwa wafugaji waliowachoma mikuki vijana wenzao.
 
igunga
Vurugu za kutaka kuchoma moto chumba hicho zilitokea juzi katika Kijiji cha Isakamaliwa baada ya makundi mawili ya wafugaji wa kata hiyo kutofautiana na kusababisha kundi moja kushambulia jingine kwa mikuki wakidaiwa kuingiza mifugo kinyume cha sheria katika bonde la Magogo.

Post a Comment Blogger

 
Top