Wahamiaji
Haramu hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole katika kata
ya Ruaha Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi likiwa katika
doria ya kawaida na kulitilia mashaka gari hilo lililokuwa limebeba
matenga ya Nyanya.
Kiongozi
wa Wahamiaji Haramu,akiwagawia wenzake mikate ilionunuliwa na
wanahabari waliokuwepo kwenye tukio hilo kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi mkoani humo.
Kiongozi
wa Wahamiaji Haramu,akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na
sakata lao la kukamatwa nchini Tanzania,anasema wamesafiri nchini kwao
Ethiopia mpaka Tanzania kwa siku 21
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akizungumza na
Waaandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye makao ya Polisi ya mkoani
humo,akithibisha kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao wakiwa katika roli
lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega
Ally (37) mkazi Tanga wakitokea nchini Ethiopia kuelekea nchini Afrika
Kusini.
Roli
lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega
Ally (37) mkazi Tanga ndilo lililotumika kuwabeba wahamiaji hao.
Matenga ya Nyanya ambamo Wahamiaji hao walikuwa wamekaa. Picha kwa hisani ya Michuzi
======= ======= ====== ========
WAHAMIAJI HARAMU 46 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI
Na Denis Mlowe,Iringa
JESHI
la Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 46
kutoka Ethiopia waliokuwa wakielekea nchini Afrika ya Kusini.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amethibitisha
kukamatwa wahamiaji hao wakiwa katika roli lenye usajili wa namba T 342
AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga..
Mungi
alisema wahamiaji hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole
katika kata ya Ruaha Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi
likiwa katika doria ya kawaida na kulitilia mashaka gari hilo.
“Jeshi
la polisi lilipata habari za kiintelejensia kuwa kuna roli limebeba
wahamiaji haramu vijana wakajipanga na kufanikiwa kuwakamata wakiwa
katika matenga ya nyanya yaliyopangwa kwa pembeni na na kufanikiwa
kuwakamata vijana hao 46 akiwemo mtoto wa miaka 17” alisema Mungi.
Alisema
kuwa dereva wa gari hilo anashikiriwa na jeshi la polisi kwa mahojiano
zaidi na kusema baadhi ya Waethiopia hao 6 kati yao wana hati ya
kusafiria (passport).
Katika
hali ya kuonyesha ukarimu kwa wageni hao haramu waandishi wa habari
walioko katika kampeni za jimbo la Kalenga wa mkoa wa Iringa na nje ya
mkoa waliwapatia msaada wa vyakula wahamiaji hao baada ya kuonyesha
wanakabiliwa na njaa kali na kiu ya maji.
Waandishi
hao wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa
Iringa (IPC), Frank Leonard walichangishana na kupatikana kiasi cha
shilingi elfu 50 na kufanikiwa kuwapatia vyakula hivyo.credit;Michuzi
Post a Comment Blogger Facebook