0

Utafiti mpya :Mtandao wa Instagram wafikisha idadi ya watumiaji milioni 400

Rapa,Drake, ni moja kati ya watumiaji milioni 400 wa mtandao wa Instagram
Rapa,Drake, ni moja kati ya watumiaji milioni 400 wa mtandao wa Instagram
Katika Mitandao ya Kijamii iliyobeba umaarufu mkubwa Duniani, upo mtandao wa Facebook ilioanzishwa February 2004, Twitter ilioanzishwa March 2006 hiyo ilikuwa miaka miwili mbele baada ya Facebook lakini mtandao wa Instagram umechukua umaarufu mkubwa sana sasahivi kwa sababu watu wengi wanapendelea kushare picha na watu wao,
‘Insta’ ilianzishwa mwaka 2010 na kuanza kupata umaarufu mdogomdogo.!!Ripoti mpya imetoka na imethibitishwa na wamiliki wa Instagram wenyewe kuwa hivi sasa inawatumiaji MILIONI 400 mpaka kufikia September 22 2015, hiyo ni ndani ya miaka mitano tangu Mtandao huo umeanzishwa.
Instagram app
Instagram app
Kwa Takwimu hizo ni kwamba mpaka sasahivi, mtandao wa Instagram umekua kwa kasi zaidi ndani ya kipindi cha miaka mitatu ambapo watumiaji wake wanakaribia kufikia hesabu ya watumiaji wa Twitter ambao wanakadiriwa kuwa MILIONI 500 Duniani kote.
Instagram ni kama ilipata nguvu zaidi na umaarufu kuanzia mwaka 2012 ambapo wamiliki wa Facebook waliinunua Instagram kwa Dola Bilioni Moja ambazo kwa TZ inagusa karibia Trilioni 2.2 kwa hesabu ya sasahivi!

Post a Comment Blogger

 
Top