Wenger kumpa talaka mke wake
Arsene Wenger ametalakiana na mkewe Annie Wenger
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameachana na mke wake, kwa mujibu wa gazeti la The Sun.
Gazeti hilo linadai kwamba Wenger na mshirika wake huyo walipewa hukumu ya kuachana na jaji mjini Paris, ikimaanisha kuwa hawaruhusu kuonana tena.
Wenger bado anatarajiwa kumhudumia kifedha Annie, The Sun liliripoti.
Chanzo kimoja kilieleza gazeti hilo kuwa, “Wamegawana mali na kukubali kugawiana fedha ili kuachana.
“Hawajawahi kuwa na furaha kwa muda, na waliamua hayo ndio maamuzi sahihi kuyafanya.
Wawili hao walikuwa katika mahusiano ya muda mrefu na walioana 2010, wana mtoto wa kike mwenye miaka 18.
Wiki chache kabla ya harusi iliripotiwa kuwa Wenger alikuwa na urafiki wa karibu na rapa wa Ufaransa Sonia Tatar, mwenye miaka 39.
Post a Comment Blogger Facebook