Rais wa Misri amsamehe mwandishi wa Al Jazeera
Rais wa Misri amemsamehe mmoja wa waandishi wa habari wa Televisheni ya Al Jazeera aliyeshtakiwa kwa kutangaza habari za uongo.
Mohamed Fahmy, raia wa Canada, anahusishwa kwenye orodha ya wafungwa 100 waliopewa msamaha na Abdul Fattah al-Sisi.
Lakini mwenzie na Fahmy, Baher Mohamed, hajatajwa kwenye orodha hiyo, pamoja na Peter Greste wa Australia ambaye aliachiwa mwezi Februari.
Walihukumiwa miaka mitatu gerezani mwezi uliopita baada ya wakosoaji wa mashtaka ya kesi zao kutoonekana.
Post a Comment Blogger Facebook