0
uganda-gay

Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa Uganda, Balozi James Mugume, amesema kuwa Uganda haitishwi na vikwazo ilivyowekewa na Marekani kama hatua ya kupinga sheria yake kali kuhusu Ushoga.
Kwa mujibu wa BBC, Balozi Mugume ameelezea kuwa serikali ya Uganda hata hivyo itafanya mazungumzo na Marekani ili kufafanua hatua waliyochukua.
Habari zinazohusiana
Amesisitiza kuwa wataieleza Marekani sheria hiyo inapinga tabia ambayo sio ya kiafrika na maadili ambayo hayakubaliki katika jamii nyingi za kiafrika.
Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa na athari kubwa kwa nchi hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii kuwa tayari sheria hiyo imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

Post a Comment Blogger

 
Top